• HABARI MPYA

  Jumanne, Mei 23, 2017

  SPORTPESA YAWAPA MILIONI 250 SINGIDA UNITED ZA UDHAMINI LIGI KUU

  Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
  KAMPUNI ya SportPesa leo imeingia mkataba wa udhamini wa mwaka mmoja na klabu ya Singida United kwa dau la Sh. Milioni 250.
  Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa Kampuni ya SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas amesema kwamba wameingia mkataba na timu hiyo kwa sababu imeonyesha nia ya kufanya vizuri katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu ujao kutokana na usajili mzuri wanaoufanya.  
  “Tumeingia mkataba na Singida United ambayo ndiyo timu ya mwisho katika udhamini wa SportPesa nchini, kutokana na timu hii kuwa na maandalizi mazuri,”amesema Tarimba.
  Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa Kampuni ya SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas (kulia) akiwa na viongozi wa Singida United leo baada ya kusaini mkataba

  Mwenyekiti huyo wa zamani wa Yanga, Tarimba amesema kwamba mkataba huo una kipengele cha kuongezwa iwapo Singida United itafanikiwa kubaki Ligi Kuu baada ya msimu ujao.
  Kwa upande wake, kocha wa Singida United, Mholanzi Hans van der Pluijm amesema kwamba udhamini huo ni chachuya timu kufanya vizuri msimu ujao.
  “Nafurahi baada ya mafanikio yangu nikiwa na Yanga, sasa Napata fursa nyingine nzuri ya kuendeleza mafanikio hayo na Singida United,”amesema.
  Mchezaji wa Singida United, Nizar Khalfan akiwa na jezi yenye nembo ya SportPesa
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SPORTPESA YAWAPA MILIONI 250 SINGIDA UNITED ZA UDHAMINI LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top