• HABARI MPYA

  Saturday, May 27, 2017

  OMOG AWAANZISHA PAMOJA MAVUGO NA LUIZO, APANGA KIKOSI MBAO WAKIPONA WAKATAMBIKE!

  Na Mwandishi Wetu, DODOMA
  KOCHA Mkuu wa Simba, Mcameroon Joseph Marius Omog amewaanzisha pamoja washambuliaji Mrundi, Laudit Mavugo na mzawa Juma Luizio katika mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), au Azam Sports Federation Cup (ASFC) jioni ya leo Uwanja wa Jamhuri, Dodoma dhidi ya Mbao FC ya Mwanza.
  Kwa ujumla, Omog amepanga kikosi cha kuutawala mchezo ili kuurahisisha ushindi, kwani amelundika viungo wanne katikati, ambao ni Nahodha Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Muzamil Yassin na Said Ndemla.
  Simba inakutana na Mbao FC kuanzia Saa 10:00 jioni ya leo kuwania tiketi ya Kombe la Shirikisho, baada ya kuzidiwa kete na mahasimu wao, Yanga SC kwenye kinyang’anyiro cha tiketi ya Ligi ya Mabingwa.
  Kocha wa Simba, Mcameroon Joseph Marius Omog amewaanzisha pamoja washambuliaji Mrundi, Laudit Mavugo na mzawa Juma Luizio

  Yanga wameipiku Simba ‘dakika za mwisho’ katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na kujikatia tiketi ya Ligi ya Mabingwa kwa mara ya tatu mfululizo, mwakani. 
  Simba ilicheza michuano ya Afrika kwa mara ya mwisho, mwaka 2013 na kutolewa na Recreativo de Lobolo ya Angola kwa vipigo vya nyumbani na ugenini, ikifungwa 1-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na 4-0 ugenini.
  Tangu hapo, Wekundu wa Msimbazi wamekuwa wakizishuhudia Azam na Yanga zikibadilisha ndege kwenda nchi mbalimbali kwa michuano ya Afrika.
  Lakini leo, Simba SC imepata nafasi nzuri ya kukata tiketi ya kurudi kwenye michuano ya Afrika baada ya miaka minne, watakapomenyana na timu ya Mbao iliyopanda Ligi Kuu msimu huu na kuweka rekodi ya kufika fainali ya ASFC.
  Kikosi kamili cha Simba leo ni; Daniel Agyei, Janvier Besala Bokungu, Mohammed Hussein ‘Tahabalala’, James Kotei, Juuko Murshid, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Muzamil Yassin, Laudit Mavugo, Said Ndemla na Juma Luizio.
  Kwenye benchi watakuwapo Dennis Richard, Vincent Costa, Abdi Banda, Mwinyi Kazimoto, Ibrahim Hajib, Frederick Blagnon na Moses Kitandu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: OMOG AWAANZISHA PAMOJA MAVUGO NA LUIZO, APANGA KIKOSI MBAO WAKIPONA WAKATAMBIKE! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top