• HABARI MPYA

  Jumatatu, Mei 29, 2017

  HAZARD MCHEZAJI BORA WA MSIMU CHELSEA, ASHINDA PIA BAO BORA

  Kiungo wa Chelsea, Eden Hazard akiwa ameshika tuzo ya Bao Bora la Msimu usiku wa jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA  


  TUZO ZA CHELSEA 2017 

  Bao Bora la Msimu: Eden Hazard
  Mchezaji Bora wa Wachezaji: N'Golo Kante 
  Mchezaji Bora wa Kike: Karen Carney
  Mchezaji Bora wa Akademi: Mason Mount
  Mchezaji Bora wa Mwaka: Eden Hazard
  Tuzo Maalum: John Terry 
  KIUNGO wa Chelsea, Eden Hazard ameshinda tena Tuzo ya Mchezaji Bora wa Msimu wa katika klabu hiyo katika sherehe zilizofanyika usiku wa jana mjini London.
  Mbelgiji, ambaye pia ameshinda tuzo ya Bao Bora la Msimu katika sherehe zilizofanyika Battersea Evolution, huku N'Golo Kante akishinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Wachezaji. 
  Kocha Antonio Conte alikabidhi tuzo hiyo kubwa, ambayo hutokana na kura za mashabiki baada ya kutolewa kwa orodha ya mwisho akiingia na Cesar Azpilicueta, David Luiz na Kante. 
  Usiku huo ukakamilishwa kwa sherehe ya kumuaga Nahodha John Terry anayestaafu, ambaye alipewa tuzo maalum kuutambua mchango wake.
  Chelsea imemaliza msimu vizuri baada ya kubeba ubingwa wa Ligi Kuu ya England na kushika nafasi ya pili kwenye Kombe la FA.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: HAZARD MCHEZAJI BORA WA MSIMU CHELSEA, ASHINDA PIA BAO BORA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top