• HABARI MPYA

  Jumatano, Mei 31, 2017

  SIMBA YATANDIKWA 2-1 NA NYUNDO KATAVI

  Na Prince Akbar, KATAVI
  WASHINDI wa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC), Simba SC leo wameshindwa kufurukuta mbele ya wenyeji, Nyundo FC baada ya kuchapwa mabao 2-1 Uwanja wa Katavi mjini Katavi katika mchezo wa kirafiki.
  Simba iliyokuwa inacheza mchezo huo kukamilisha msimu kabla ya kuvunja kambi na kuwapa wachezaji wake mapumziko, ilikwenda mapumziko ikiwa tayari imekwishachapwa 2-0.
  Juma Luizio ameifungia Simba bao la kufutia machozi ikilala 2-1 mbele ya Nyundo

  Lakini kipindi cha pili, kocha aliyeiongoza timu leo, Nico Kiondo wa timu B alimuingiza Meneja wa timu, Mussa Hassan Mgosi kwenda kuchukua nafasi ya chipukizi wa timu ya vijana, Mohammed Mussa na ndipo hapo Simba ikapata uhai hata kufanikiwa kupata bao la kufutia machozi.
  Mgosi aliichachafya ngome ya Nyundo na kufumua shuti kali, ambalo kipa wa Nyundo alitema na kumkuta mshambuliaji Juma Luizio aliyeukwamisha mpira nyavuni.  
  Baada ya mchezo huo, kikosi cha Simba kinatarajiwa kurejea Dar es Salaam mapema kesho.
  Kikosi kilichcheza Simba leo ni; Ally Salum/Dennis Rochard dk46, Kevin Faru, Joseph Antony, Vincent Costa, Freddy Anthony, Mokiwa Pelusi, Mohammed Mussa/Mussa Mgosi dk80, Rashid Juma, Frederick Blagnon/Moses Kitandu dk46, Juma Luizo na Ally Abdallah.   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA YATANDIKWA 2-1 NA NYUNDO KATAVI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top