• HABARI MPYA

  Jumapili, Mei 28, 2017

  CARRICK EXTENDS CONTRACT TO JUNE 2018

  KLABU ya Manchester United imemuongezea mkataba wa mwaka mmoja kiungo wake, Michael Carrick hadi Juni 2018.
  Carrick, mwenye umri wa miaka 35, alisajiliwa United Julai mwaka 2006 na katika kipindi chake cha kuwa na klabu hiyo ameshinda mataji matano ya Ligi Kuu ya England, Kombe la FA, mawili ya Kombe la Ligi, Kombe la Klabu Bingwa ya Dunia la FIFA, Ligi ya Mabingwa Ulaya, Ngao ya Jamii mara sita na hili la karibuni la Europa League.
  "Kwa namna nzuri tulivyomaliza msimu, kwa taji jipya kwenye kabati letu, nina furaha safari yangu na klabu hii inakwenda kuendelea," alisema Carick.
  Kwa uopande wake, kocha Mreno Jose Mourinho alisema: 
  "Nimefurahia kufanya kazi na Michael kwa msimu huu uliokwisha. Ni mmoja wa wachezaji wa kweli wa kulipwa wa mchezo. Siyo tu ni mchezaji mkubwa, pia ni binadamu mkubwa na mfano mkubwa wa kuigwa kwa wachezaji wetu chipukizi,".
  "Nina furaha ameongeza mkataba na ningependa kuchukua fursa hii kumtakia Michael kila la heri katika mechi yake maalum ya kumuaga Jumapili ijayo,".
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CARRICK EXTENDS CONTRACT TO JUNE 2018 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top