• HABARI MPYA

  Tuesday, May 23, 2017

  CONTE ABEBA TUZO MBILI ZA UKOCHA BORA ENGLAND

  KOCHA wa Chelsea, Antonio Conte ameshinda tuzo mbili za Chama cha Makocha wa Ligi England.
  Mtaliano huyo ameshinda tuzo ya Kocha Bora wa Mwaka na Kocha Bora wa Ligi Kuu, after baada ya kuwapa ubingwa The Blues katika msimu wake wa kwanza.
  Kocha wa Brighton, Chris Hughton ameshinda tuzo ya Kocha Bora wa Championship baada ya kuiwezesha timu hiyo kupanda Ligi Kuu.
  Chris Wilder wa Sheffield United na Paul Cook wa Portsmouth, wamepata tuzo za Ukocha Bora wa Ligi Daraja la Kwanza na la Pili.
  Kocha wa Chelsea, Conte ambaye timu yake imeshinda mechi 30 za Ligi Kuu ambayo ni rekodi, anaweza kumaliza msimu na mataji mawili iwapo ataifunga Arsenal katika fainali ya Kombe la FA Jumamosi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CONTE ABEBA TUZO MBILI ZA UKOCHA BORA ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top