• HABARI MPYA

  Jumatatu, Mei 29, 2017

  BEKI MGHANA WA MBAO AIKATAA SINGIDA UNITED ATUE AZAM

  Na Shekha Jamal, DODOMA
  BEKI wa Mbao FC, Asante Kwasi amesema kwamba amekataa kujiunga na Singida United ili kusubiri uwezekano wa kusajiliwa na Azam  kwa msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online jana, Kwasi alisema kwamba kwa sasa yeye ni mchezaji huru hivyo yupo tayari kutumikia timu yoyote kikubwa anaangalia maslah.
  Kwasi ambaye ni mchezaji huru kwa sasa baada ya kumaliza mkataba wake Mbao FC, alisema kocha wa Singida United, Hans van der Pluijm amempa ofa ya kujiunga na timu yake iliyopanda Ligi Kuu msimu huu, lakini amekataa.
  Asante Kwasi amesema amekataa ofa ya Singida United ili kusubiri uwezekano wa kusajiliwa na Azam  

  Alisema wakala wake, ambaye anaishi Afrika Kusini ndiye anayeshughulikia mipango yake yote na ndiye anayeweza kuzungumza zaidi.
  "Ninaipenda Azam kutokana na inavyoendeshwa kisasa, natamani siku moja nichezee timu hiyo, kama timu nyingine zitakuja na dau nzuri basi sina budi kusaini," alisema raia huyo wa Ghana.
  Kwasi amekuwa na msimu mzuri Mbao FC akiiwezesha kubaki Ligi Kuu katika msimu wake wa kwanza baada ya kupanda na pia kufika Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) ambako walifungwa na Simba 2-1.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BEKI MGHANA WA MBAO AIKATAA SINGIDA UNITED ATUE AZAM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top