• HABARI MPYA

  Jumanne, Mei 30, 2017

  KROENKE AMBAKIZA WENGER ARSENAL KWA MIAKA MINGINE MIWILI


  Arsene Wenger amemuambia Stan Kroenke atabaki Arsenal baada ya kumaliza mkataba wake wa sasa PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  MATAJI ALIYOSHINDA WENGER ARSENAL  

  Ligi Kuu (3): 1997–98, 2001–02, 2003–04
  Kombe la FA (7): 1997–98, 2001–02, 2002–03, 2004–05, 2013–14, 2014–15, 2016–17  
  KOCHA Arsene Wenger amemuambia mmiliki wa Arsenal, Stan Kroenke nia yake kutaka kuendelea kuwa kocha wa klabu hiyo.
  Habari hizo zimeifikia bodi ya The Gunners katika kikao chake cha leo Jumanne.
  Inamaanisha kwamba Wenger atasaini mkataba mpya wa miaka miwili.
  Kroenke, aliyehudhuria fainali ya Kombe la FA Jumamosi Arsenal ikishinda 2-1 dhidi ya Chelsea Uwanja wa Wembley, London, amezungumza na Wenger zaidi ya saa 72 zilizopita. 
  Mfaransa huyo inafahamika amemuambia mwana hisa mkubwa wa klabu hiyo nia yake ya kubaki na Kroenke ndiye haswa anayemkingia kifua asing'oke.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KROENKE AMBAKIZA WENGER ARSENAL KWA MIAKA MINGINE MIWILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top