• HABARI MPYA

  Sunday, May 28, 2017

  YANGA YAFUNGA MSIMU NA USHINDI MNONO ARUSHA

  Na Mwandishi Wetu, ARUSHA
  YANGA SC imefunga msimu kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji, AFC kwenye mchezo wa kirafiki jioni ya leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.
  Winga Geoffrey Mwashiuya amefunga mabao mawili leo, la kwanza dakika ya 24 na la pili dakika ya 67, kabla ya mshambuliaji wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Samuel Greyson kufunga la tatu dakika ya 90.
  Kocha Msaidizi, Juma Mwambusi alikiongoza kikosi leo baada ya bosi wake, Mzambia George Lwandamina kubaki Dar es Salaam.
  Geoffrey Mwashiuya amefunga mabao mawili leo Yanga ikiilaza 3-0 AFC mjini Arusha

  Na Mwambusi akawapa nafasi vijana wanne wa timu B, beki Mohammed Ally, viungo Maka Edward, Yussuf Mhilu na mshambuliaji Festo Greyson, ambao wote walicheza vizuri.
  Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kurejea Dar es Saaam kesho na baada ya hapo wachezaji watakuwa na kikao na uongozi kabla ya kupewa likizo ya baada ya msimu. 
  Kikosi cha Yanga leo kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’/Deo Munishi ‘Dida’ dk76, Pato Ngonyani, Mohammed Ally, Vincent Bossou, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Maka Edward, Yussuf Mhilu, Juma Mahadhi/Festo Greyson dk75, Matheo Anthony, Emmanuel Martin/Samuel Greyson dk64 na Geoffrey Mwashiuya. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAFUNGA MSIMU NA USHINDI MNONO ARUSHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top