• HABARI MPYA

  Ijumaa, Septemba 30, 2016

  MAZOEZI YA MWISHO YA SERENGETI BOYS KABLA YA KUIVAA KONGO JUMAPILI

  Kiungo wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, Kelvin Nashon ‘akisepa na kijiji cha mabeki’ wakati wa mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat - Rais wa zamani wa Congo kabla ya mchezo wa Jumapili.
  Libero wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, Ally Msengi (Kulia) akimiliki mpira huku Mshambuliaji wa timu hiyo, Ibrahim Abdallah akipigia hesabu mpira huo wakati wa mazoezi yaliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat
  Beki wa kushoto wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, Nickson Kibabage akimdhibiti Kelvin Nashon wakati wa mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Déba
  Mshauri wa Maendeleo ya soka la Vijana, Kim Poulsen (kushoto) akimwelezea Mkuu wa Msafara wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, Ayoub Nyenzi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat - Rais wa zamani wa Congo.
  Muhsin Malima Makame au unaweza ukamwita ‘Super Sub’ wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, akikokota mpira kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat 
  Kipa Na. 1 wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, Ramadhani Kabwili akifanya vitu vyake kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAZOEZI YA MWISHO YA SERENGETI BOYS KABLA YA KUIVAA KONGO JUMAPILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top