• HABARI MPYA

  Jumamosi, Septemba 24, 2016

  SIMBA YAENDA MORO KUJIANDAA NA YANGA, HAJIB HATARINI KUKOSA PAMBANO LA WATANI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC inakwenda kambini kesho mjini Morogoro kesho kujiandaa na mchezo dhidi ya mahasimu, Yanga – lakini kocha Mcameroon Joseph Marius Omog hana uhakika wa kumtumia mshambuliaji Ibrahim Hajib Migomba siku hiyo.
  Simba SC itamenyana na Yanga SC Oktoba 1, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na leo Hajib alishindwa kumaliza mchezo dhidi Maji Maji. 
  Hajib aliondoka uwanjani baada ya dakika 21 tu kufuatia kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na kiungo Said Ndemla.
  Hajib akiondoka uwanjani dakika ya 21 tu baada ya kuumia 
  Pamoja na kucheza kwa muda mfupi, lakini Hajib aliwahenyesha mabeki wa Maji Maji
  Hajib akiwa amekaa chini baada ya kuumia
  Wachezaji wa Simba na Daktari wakimjulia hali Hajib baada ya kuumia
  Hajib akiondoka uwanjani baada ya kuumia
  Hajib akipokewa na wenzake wa benchi
  Hajib akiwa ameketi na wachezaji wa akiba wa Simba

  Pamoja na kumpoteza mapema Hajib, Simba SC ilifanikiwa kushinda 4-0 jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam -mabao ya Jamal Simba Mnyate na Shizza Ramadhani Kichuya kila mmoja mawili.
  Hajib aliondoka uwanjani akichechemea na kwenda kuungana na wachezaji wa akiba benchi kushuhudia sehemu iliyobaki ya mchezo.
  Na hata baada ya mchezo wakati wachezaji wa Simba wanakwenda kupanda basi lao kuondoka, bado Hajib alionekana kuchechemea.
  Simba SC iliyofikisha pointi 16, baada ya mechi ya sita leo, wakishinda tano na sare moja watahitaji ushindi dhidi ya Yanga pia wiki ijayo, ili kuzidi kuongoza mbio za ubingwa. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA YAENDA MORO KUJIANDAA NA YANGA, HAJIB HATARINI KUKOSA PAMBANO LA WATANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top