• HABARI MPYA

  Jumatano, Septemba 21, 2016

  BOCCO MCHEZAJI BORA WA LIGI KUU AGOSTI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa Azam FC, John Raphael Bocco 'Adebayor' amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom wa mwezi Agosti kwa msimu wa 2016/2017.
  Bocco ambaye pia ni nahodha wa Azam FC aliwashinda wachezaji Mzamiru Yasin wa Simba na Said Kipao wa JKT Ruvu. Katika mechi mbili ilizocheza katika mwezi huo, Bocco aliifungia  timu yake mabao matatu likiwemo la kusawazisha dhidi ya African Lyon.
  John Bocco amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Agosti

  Alifunga mabao mengine mawili kwenye ushindi wa mabao 3-0 wa timu yake dhidi ya Majimaji. Katika mechi hizo mbili, Azam FC ilifanikiwa kupata pointi nne kati ya sita.
  Mwezi huo ulikuwa na raundi mbili tu za Ligi hiyo iliyoanza kutimua vumbi Agosti 20 mwaka huu. Kwa kushinda tuzo hiyo, Bocco atazawadiwa kitita cha sh. milioni moja kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom Tanzania.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BOCCO MCHEZAJI BORA WA LIGI KUU AGOSTI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top