• HABARI MPYA

  Jumamosi, Septemba 24, 2016

  NDANDA YAITOTESHA AZAM 2-1, MBAO YATOA SARE 1-1 NA MTIBWA MANUNGU

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  NDANDA FC imewaangusha washindi wa Ngao ya Jamii Azam FC kwa mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Nangwanda SIjaona, Mtwara leo.
  Mabao ya Ndanda yamefungwa na Riffat Khamis na Hajji Mponda, wakati la Azam FC lilifungwa na Nahodha John Raphael Bocco.
  Hicho kinakuwa kipigo cha pili mfululizo kwa Azam FC baada ya wiki iliyopita kufungwa 1-0 na Simba SC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
  Matokeo hayo yanaifanya Azam FC ibakie na pointi zake 10 baada ya kucheza mechi sita, wakifungwa mbili, sare moja na kushinda tatu.
  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, JKT Ruvu wameshinda 2-0 dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani, Prisons wametoka sare ya 0-0 na Mwadui Uwanja wa Sokoine, Mbeya na Mtibwa Sugar imelazimishwa sare ya 1-1 na Mbao FC Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro.
  Ligi Kuu inaendelea kesho kwa mechi mbili; Ruvu Shooting na Toto Africans Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani, Stand United na Yanga SC Uwanja wa Kambarage, Shinyanga na kesho African Lyon itamenyana na Kagera Sugar Uwanja wa Taifa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NDANDA YAITOTESHA AZAM 2-1, MBAO YATOA SARE 1-1 NA MTIBWA MANUNGU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top