• HABARI MPYA

  Alhamisi, Septemba 22, 2016

  MOURINHO NA PEP TENA; MAN UNITED YAPANGWA NA MA CITY KOMBE LA LIGI MWEZI UJAO

  Jose Mourinho (kushoto) na Pep Guardiola (kulia) watakutana tena wakati United itakapoivaa City kwenye Kombe la Ligi England mwezi Oktoba

  RAUNDI YA NNE KOMBE LA LIGI ENGLAND;

  West Ham vs Chelsea
  Manchester United vs Manchester City 
  Arsenal vs Reading
  Liverpool vs Tottenham 
  Bristol City vs Hull City
  Leeds United vs Norwich City
  Newcastle vs Preston North End
  Southampton vs Sunderland 
  (Mechi zitachezwa Oktoba 24, mwaka huu)
  MAKOCHA wenye upinzani mkali, Jose Mourinho wa Manchester United na Pep Guardiola wa Manchester City watakutana tena katika Raundi ya Nne  ya Kombe la Ligi England (EFL Cup).
  Klabu zote za Manchester zilifuzu Jumatano usiku kwa United kuifunga Northampton na City kushinda dhidi ya Swansea kabkla ya droo ya hatua inayofuata kuzikutanisha zenyewe.
  Upinzani na wawili hao unaanzia Hispania wakati Mourinho alipokuwa anakochi Real Madrid na Guardiola Barcelona. 
  Kwa England huo utakuwa mchezo wa pili kuwakutanisha wakubwa hao wawili, baada ya awali Guardiola kuiongoza Man City kuifunga United 2-1 Septemba 10, Uwanja wa Old Trafford.
  Na sasa macho yote yataelekzwa tena Uwanja wa old Trafford Oktoba miamba hiyo ikimenyana.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MOURINHO NA PEP TENA; MAN UNITED YAPANGWA NA MA CITY KOMBE LA LIGI MWEZI UJAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top