• HABARI MPYA

  Jumatano, Septemba 21, 2016

  RAIS MAGUFULI AWAPONGEZA KILI QUEENS KWA KOMBE LA CHALLENGE

  Na Mwandishi Wetu, JINJA
  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Joseph Magufuli ameipongeza timu ya taifa ya wanawake, Kilimanjaro Queens kwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kenya jioni ya jana Uwanja wa Ufundi, Jinja.
  Katika barua yake, Rais Magufuli amesema amefurahishwa na ubingwa huo na akawaomba wachezaji wa Kilimanjaro Queens kuutumia ushindi huo kama changamoto ya kutwaa mataji zaidi ya michuano mingine.
  Ushindi wa jana ulitokana na mabao ya Mwanahamisi Omar ‘Gaucho’ na Stumai Abdallah dhidi ya moja la Kenya, lililofungwa na Christine Nafula.


  Kikosi cha Kilimanjaro Queens jana Uwanja wa Ufundi, Jinja, Uganda

  Awali, Tanzania Bara iliongoza Kundi B baada ya kushinda kura ya sarafu kufuatia sare ya 0-0 na Ethiopia katika mchezo wa mwisho wa kundi hilo, hivyo kufungana nayo kwa pointi na wasatani wa mabao kileleni. 

  Kilimanjaro Queens ilianza vizuri michuano hiyo kwa kuibamiza 3-2 Rwanda, mabao yake yakifungwa na Asha Rashid ‘Mwalala’ dakika za 11 na 65 na Stumai Abdallah dakika ya 28, wakati ya wapinzani wao yalifungwa na Ibangarrue Marie na Amina Ally wa Tanzania Bara aliyejifunga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RAIS MAGUFULI AWAPONGEZA KILI QUEENS KWA KOMBE LA CHALLENGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top