• HABARI MPYA

  Jumamosi, Septemba 24, 2016

  KIPRE TCHETCHE AREJEA OMAN KUPIGANIA UHAMISHO WAKE AZAM FC

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM 
  MSHAMBULIAJI Kipre Herman Tchetche amerejea Oman kupigania uhamisho wa kuanza kuichezea klabu yake mpya, Al-Nahda Al-Buraimi kutoka Azam FC ya Tanzania.
  Tchetche alilazimika kurejea kwao, Ivory Coast mapema mwezi huu baada ya Azam FC kugoma kumruhusu kujiunga na Al Nahda bila dola za Kimarekani 50,000.
  Na Azam ilifanya hivyo kwa sababu Tchetche aliondoka Dar es Salaam akiwa amebakiza Mkataba wa mwaka mmoja baada ya kuichezea klabu hiyo tangu mwaka 2010.  
  Kipre Tchetche amerejea Oman kupigania uhamisho wake kutoka Azam FC 

  Hata hivyo, akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE leo kutoka Muscat, Oman, Tchetche amesema anatarajia kumalizana na Azam FC ndani ya muda mfupi tangu sasa. “Tayari nimerudi Oman na ninatarajia kumalizana na Azam muda si mrefu ili nianze kucheza hapa,”alisema.    
  Kipre Tchetche alijiunga na Azam FC mwaka 2011 kwa pamoja na pacha wake, Kipre Michael Balou baada ya wote kung’ara katika kikosi cha Ivory Coast kilichokuja kucheza michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Challenge) Dar es Salaam. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KIPRE TCHETCHE AREJEA OMAN KUPIGANIA UHAMISHO WAKE AZAM FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top