• HABARI MPYA

  Jumatatu, Septemba 26, 2016

  NI MO BEJAIA NA TP MAZEMBE FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO

  MO Bejaia ya Algeria imefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika licha ya sare ya 1-1 jana usiku Uwanja wa Prince Moulay Abdallah mjini Rabat, Morocco dhidi ya wenyeji, FUS Rabat.
  MO Bejaia inakwenda fainali kwa faida ya bao la ugenini, baada ya kulazimisha sare ya 0-0 kwenye mchezo wa kwanza nyumbani Algeria.
  Katika mchezo wa jana, Mohammed Nahiri alianza kuifungia FUS Rabat dakika ya 73, kabla ya Faouzi Rahal kuisawazishia MO Bejaia dakika ya 90.
  MO Bejaia itamenyana na TP Mazembe katika Fainali ya Kombe la Shirikisho mwaka huu

  Na kwa matokeo hayo, fainali ya Kombe la Shirikisho mwaka huu itazikutanisha timu za Kundi A tupu, Mazembe na MO Bejaia, ambazo zilizipiku Yanga SC ya Tanzania na Medeama SC ya Ghana kwenda Nusu Fainali.
  Ikumbukwe mapema jana, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ilifanikiwa kwenda fainali baada ya sare ya 0-0 na Etoile du Sahel ya Tunisia mjini Lubumbashi.
  Mazembe pia imefuzu kwa faida ya bao la ugenini, baada ya kutoa sare ya 1-1 ugenini katika mchezo wa kwanza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NI MO BEJAIA NA TP MAZEMBE FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top