• HABARI MPYA

  Alhamisi, Septemba 29, 2016

  MKWASA AITA WACHEZAJI 24 KUIVAA ETHIOPIA OKTOBA 8 ADDIS

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa ametaja majina ya nyota 24 watakaounda kikosi ambacho kitasafiri mwishoni mwa wiki ijayo kwenda Addis Ababa, Ethiopia kucheza na wenyeji wetu kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika Oktoba 8, mwaka huu.
  Mkwasa maarufu kwa jina la Master amesema wachezaji aliowaita wataingia kambini Oktoba 2, 2016 kabla ya kuanza kukiandaa kuanzia Oktoba 3, 2016 ikiwa mara baada ya michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara ya mwishoni mwa wiki hii ambako Mwadui itacheza na Azam huku Mbao ikishindina na JKT Ruvu Oktoba 2, mwaka huu.
  Kocha wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa ameita wachezaji 24 kwa ajili ya mchezo dhidi ya Ethiopia Oktoba 8, mwaka huu mjini Addis Ababa

  Nyota wa Stars walioitwa na Mkwasa ni Makipa; Deogratius Munishi 'Dida' (Yanga SC), Said Kipao (JKT Ruvu) na Aishi Manula (Azam FC).
  Mabeki; Shomari Kapombe (Azam FC), Juma Abdul, Andrew Vincent, Mwinyi Hajji (Yanga SC), Mohamed Hussein 'Tshabalala' (Simba SC), David Mwantika (Azam FC) na James Josephat (Prisons).
  Viungo ni Himid Mao (Azam FC), Mohammed 'Mo' Ibrahim, 
  Jonas Mkude, Muzamil Yassin, Jamal Mnyate, Shiza Kichuya (Simba SC), Simon Msuva, Juma Mahadhi (Yanga SC) na Hassan Kabunda (Mwadui FC).
  Washambuliaji ni Ibrahim Hajib (Simba SC), John Bocco (Azam FC), Mbwana Samatta KRC Genk (Ubelgiji), Elius Maguli (Oman) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).
  Mchezo huo ulio katika kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), utafanyika mjini Addis Ababa, baada ya maombi ya Shirikisho la Soka Ethiopia (EFF).
  Hii ni faida kwa Tanzania kama itashinda mchezo huo kwa maana kina alama za nyongeza kama inatokea unaifunga timu mwenyeji.
  Matokeo ya mchezo huo, ni sehemu malumu kupima viwango vya ubora na uwezo wa timu za taifa. Kwa sasa Tanzania inashika nafasi ya 132 kati ya nchi 205 wanachama wa FIFA zilizopimwa ubora. Ethiopia yenyewe inashika nafasi ya 126.
  Argentina inaongoza ikifuatiwa na Ubelgiji anakocheza Mbwana Samatta – nyota wa kimataifa wa Tanzania. Samatta anacheza klabu ya K.R.C Genk inayoshiriki Ligi Kuu ya Ubelgiji. Timu nyingine bora kimataifa ni Ujerumani, Colombia na Brazil.
  Katika Bara la Afrika, Ivory Coast ambayo ni ya 34 kwa ubora duniani ndiyo inayoongoza ikifuatiwa na Algeria, Senegal, Tunisia na Ghana.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MKWASA AITA WACHEZAJI 24 KUIVAA ETHIOPIA OKTOBA 8 ADDIS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top