• HABARI MPYA

  Jumapili, Septemba 25, 2016

  YANGA SC KUENDELEZA UBABE SHINYANGA LEO?

  Na Mwandishi Wetu, SHINYANGA
  MABINGWA watetezi, Yanga SC leo watakamilisha mechi zao za Shinyanga kwa kumenyana na Stand United Uwanja wa Kambarage mjini hapa katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Yanga ambayo ilishinda 2-0 wiki iliyopita katika mchezo wa kwanza hapa dhidi ya Mwadui FC, inahitaji ushindi leo ili kuendelea kwafukuzia mahasimu wao wa jadi, Simba SC kileleni. 
  Kocha Mholanzi wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema anafurahi washambuliaji wake wazoefu Mrundi Amissi Tambwe na Mzimbabwe Donald Ngoma wako fiti kuelekea mchezo huo.

  Ligi Kuu iliendelea jana, Simba SC ikiichapa 4-0 Maji Maji ya Songea Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mabao ya Shizza Kichuya na Jamalk Mnyate kila mmoja mawili, Ndanda FC ilishinda 2-1 dhidi ya Azam FC Uwanja wa Nangwanda SIjaona, Mtwara.
  Mechi nyingine za Ligi Kuu jana, JKT Ruvu walishinda 2-0 dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani, Prisons walitoka sare ya 0-0 na Mwadui Uwanja wa Sokoine, Mbeya na Mtibwa Sugar ililazimishwa sare ya 1-1 na Mbao FC Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro.
  Ligi Kuu inaendelea leo kwa mechi mbili; Mbali na Stand United na Yanga SC Uwanja wa Kambarage, Shinyanga – na Ruvu Shooting itamenyana na Toto Africans Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani na kesho African Lyon itamenyana na Kagera Sugar Uwanja wa Taifa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC KUENDELEZA UBABE SHINYANGA LEO? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top