• HABARI MPYA

  Jumanne, Septemba 27, 2016

  KAVUMBANGU APATA TIMU ETHIOPIA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa zamani wa Yanga na Azam FC, Didier Kavumbangu amejiunga na klabu Shirika la Umeme Ethiopia (EEPCO) kwa mkataba wa mwaka mmoja.
  Kavumbangu amejiunga na klabu hiyo kwa msaada wa wakala maarufu wa wachezaji wa Afrika, Mganda Gibby Kalule ambaye ne Meneja wake kwa sasa.
  “Kabumbangu yupo hapa Ethiopia kwa sasa, amesaini klabu ya EEPCO na kuanza maisha mapya mara moja, “alisema Kalule.
  Didier Kavumbangu (kulia) amejiunga na klabu ya EEPCO ya Ethiopia

  Kavumbangu aliyezaliwa Mei 2, mwaka 1988 mjini Bujumbura, Burundi, amejiunga na EEPCO akitokea Azam FC aliyoichezea kwa misimu miwili baada kujiunga nayo kutoka Yanga SC.
  Awali ya hapo, Kavumbangu alichezea Lydia Ludic Burundi Academic (LLB), Atletico Olympic ya kwao na TP Mazembe ya DRC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KAVUMBANGU APATA TIMU ETHIOPIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top