• HABARI MPYA

  Jumatano, Septemba 21, 2016

  MICHO AWAITA WOTE, OKWI, KIIZA NA JUUKO THE CRANES

  Na Mwandishi Wetu, KAMPALA
  KOCHA wa timu ya taifa ya Uganda, Milutin Sredojevic 'Micho' amewajumuisha wote, beki wa Simba SC, Juuko Murshid na mshambuliaji Emmanuel Okwi anayecheza Denmark katika kikosi chake kitakachocheza mechi mbili mwezi ujao.
  Micho, kocha wa zamani wa Yanga SC, leo amekutana na Waandishi wa Habari makao makuu ya Shirikisho la Soka Uganda (FUFA), maarufu kama FUFA House eneo la Mengo, Kampala na kutaja kikosi kitakachomenyana na Togo katika mechi ya kirafiki ya kimataifa kujiandaa na ya kufuzu Kombe la Dunia 2018 dhidi ya Ghana.
  Okwi ameitwa kwenye kikosi cha Uganda kitakachocheza na Togo na Ghana mwezi ujao

  Micho aliongozana na Rais wa FUFA, Mhandisi Moses Magogo, Ofisa wa The Cranes, Patrick Ntege na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa FUFA, Ahmed Hussein na akawapongeza wachezaji kwa kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani Gabon.
  Uganda Cranes itacheza na Togo Oktoba 4 katika mchezo wa kirafiki mjini Lome, kabla ya kumenyana na Ghana katika mchezo wa Kundi E mjini Tamale City kuwania tiketi ya fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018.
  Wachezaji wa nyumbani wataanza mazoezi Oktoba 1 mwaka 2016 baada ya mechi za Ligi Kuu ya Azam Uganda Septemb 30, wakati wachezaji wengi wa kigeni wataungana na timu moja kwa moja mjini Lome.
  Kikosi kamili cha Uganda alichotaja Micho leo kinaundwa na makipa; Dennis Onyango (Mamelodi Sundowns, Afrika Kusini), Salim Jamal (El Merriekh, Sudan), Benjamin Ochan (KCCA, Uganda) na Ismail Watenga (Vipers, Uganda).
  Mabeki; Nicholas Wadada (Vipers, Uganda), Dennis Iguma (Al Ahed, Lebanon), Joseph Nsubuga (SC Villa, Uganda),  Isaac Isinde, Murushid Jjuuko (Simba, Tanzania), Rashid Toha (Onduparaka, Uganda), Timothy Awany (KCCA, Uganda), Halid Lwaliwa (Vipers, Uganda), Joseph Ochaya (KCCA, Uganda), Godfrey Walusimbi (Gor Mahia, Kenya)
  Viungo; Mike Azira (Colorado Rapids, Uganda), Geofrey ‘Baba’ Kizito (Than Quảng Ninh, Vietnam), Aucho Khalid (Baroka, Afrika Kusini), Ivan Ntege (KCCA, Uganda), Moses Oloya (Kuban Krasnodar, Urusi), Tonny Mawejje (Knattspyrnufélagið Þróttur, Iceland), William Luwagga Kizito (Rio Ave, Ureno) na Abdulmalick Vitalis Tabu (SC Villa, Uganda).
  Washambuliaji ni: Hamis ‘Diego’ Kizza (Free State Stars, Afrika Kusini), Geofrey Massa (Baroka, Afrika Kusini), Emmanuel Arnold Okwi (Sondjerskey, Denmark), Yunus Sentamu (Ilves, Finnland), Farouk Miya (Standard Liege, Denmark), Erisa Ssekisambu (Vipers, Uganda), Muhammed Shaban (Onduparaka, Uganda), Edrisa Lubega (Proline, Uganda)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MICHO AWAITA WOTE, OKWI, KIIZA NA JUUKO THE CRANES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top