• HABARI MPYA

  Alhamisi, Septemba 29, 2016

  SIMBA, YANGA ZAREJEA KESHO DAR TAYARI KWA KIPUTE CHA JUMAMOSI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  WATANI wa jadi, Simba na Yanga wote wanatarajiwa kurejea kesho Dar es Salaam kutoka kwenye kambi zao Morogoro na Pemba tayari kwa mchezo wa Jumamosi.
  Miamba hiyo ya soka ya Tanzania inatarajiwa kuumana Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Simba SC inatokea Morogoro na Yanga inatokea Pemba, ambako kila timu ilikwenda kuweka kambi ya takriban wiki moja kujiandaa na mchezo huo.
  Timu hizo zitakutana Simba SC ikiwa inaongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 16 baada ya kucheza mechi sita, ikishinda tano na sare moja, wakati Yanga ni ya tatu kwa pointi zake 10 za mechi tano, ikiwa imeshinda tatu, sare moja na kufungwa moja.   
  Simba itahitaji ushindi Jumamosi ili kufuta uteja wa kufungwa mechi zote za msimu uliopita 2-0 kila mchezo, wakati Yanga pamoja na kutaka kuendeleza ubabe, lakini pia itahitaji kushinda ili kujiweka sawa katika mbio za ubingwa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA, YANGA ZAREJEA KESHO DAR TAYARI KWA KIPUTE CHA JUMAMOSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top