• HABARI MPYA

  Alhamisi, Septemba 22, 2016

  HOMA YA PAMBANO LA WATANI… MAMA LORAA AWAAHIDI ‘MADOLA’ WACHEZAJI YANGA WAKIUA MNYAMA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SHABIKI na mwanachama maarufu wa Yanga, Catherine Ambakisye ‘Mama Loraa’ amewaahidi dola za Kimarekani wachezaji wa Yanga wakiifunga Simba wiki ijayo.
  Watani wa jadi katika soka la Tanzania, Simba na Yanga watakutana Oktoba 1, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Na Mama Loraa katika kuwahamasisha wachezaji wa Yanga, ametenga dola 600 za Kimarekani, zaidi ya Sh. Milioni 1.2 kwa ajili ya zawadi wachezaji iwapo watamfunga mtani.
  Mama Loraa (kushoto) akiwa na Baby Madaha (katikati) na Isabella Mpanda (kulia)
  “Mimi ni shabiki wa Yanga damu. Nimeona umuhimu wa mechi ya Oktoba 1 (2016 dhidi ya Simba). Hivyo nikaona nitoe chochote kidogo kuchochea morali. Nina imani hiki kidogo nimeahidi, lakini morali inaweza kuwa kubwa. Ninaomba Yanga washinde,”amesema.

  Akifafanua, Mama Loraa alisema kwamba ametenga dola 600 kununua hadi mabao matatu yatakayofungwa na wachezaji wa Yanga, kila moja kwa dola 200.
  Lakini Mama Loraa amesema atatoa zawadi hiyo iwapo tu Yanga itashinda au kutoa sare, lakini hatatoa hata senti moja iwapo itafungwa hata 2-1, 3-2, 4-3.
  “Washinde hata iwe 3-2 nitanunua kila bao kwa dola 200,”amesema na kuwataka wapenzi wengine na wanachama wa Yanga kujitokea kuongeza ofa zao ilio kuwahamasisha wachezani wa timu yao wawafunge mahasimu Oktoba 1, Uwanja wa Taifa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: HOMA YA PAMBANO LA WATANI… MAMA LORAA AWAAHIDI ‘MADOLA’ WACHEZAJI YANGA WAKIUA MNYAMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top