• HABARI MPYA

  Jumatatu, Septemba 26, 2016

  MRWANDA AING’ARISHA KAGERA SUGAR, YAILAZA 2-0 AFRICAN LYON

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  KAGERA Sugar imeizima African Lyon nyumbani, kwa kuichapa mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Shukrani kwao wafungaji wa mabao hayo, Danny Mrwanda dakika ya 40 na Suleiman Mangoma dakika ya 43 na sasa Kagera Sugar inayofundishwa na Mecky Mexime inafikisha pointi tisa baada ya mechi sita.
  Danny Mrwanda ameifungia Kagera Sugar ikiibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya African Lyon 

  Kagera imevuna pointi hizo kutokana na kushinda mechi mbili, sare tatu na kufungwa moja, wakati Lyon inabaki na pointi zake sita baada ya mechi sita. 
  Mechi hiyo ilikuwa inakamilisha mzunguko ulioanza wikiendi, JKT Ruvu ikiifunga 2-0 
  Mbeya City Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani, Simba ikiilaza 4-0 Maji Maji Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Ndanda ikiilaza 2-1 Azam FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara, Prisons ikilazimishwa sare ya 0-0 na Mwadui FC Uwanja wa Sokoine, Mbeya na Mtibwa Sugar ikilazimishwa sare ya 1-1 na Mbao FC Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro Jumamosi.
  Mechi nyingine zilichezwa Jumapili, Ruvu Shooting ikalazimishwa sare ya 0-0 na Toto Africans Uwanja wa Mabatini na Stand United ikawafunga mabingwa watetezi, Yanga 1-0 Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MRWANDA AING’ARISHA KAGERA SUGAR, YAILAZA 2-0 AFRICAN LYON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top