• HABARI MPYA

  Ijumaa, Septemba 23, 2016

  SIMBA SC YAWAAMBIA MAJIMAJI KIFO LAZIMA TU KESHO WATAKE WASITAKE

  RATIBA YA LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA…
  Septemba 24, 2016
  JKT Ruvu Vs Mbeya City
  Simba Vs Maji Maji
  Ndanda Vs Azam FC
  Prisons Vs Mwadui
  Mtibwa Sugar Vs Mbao
  Septemba 25, 2016
  Ruvu Shooting Vs Toto Africans
  Stand United Vs Yanga SC
  African Lyon Vs Kagera Sugar

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  WAKATI Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inaendelea kesho, Simba SC imewaambia Maji Maji watakufa wapende wasipende.
  Simba SC watakuwa wenyeji wa Maji Maji kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mfululizo wa ligi hiyo na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Hajji Sunday Manara amesema; “Ushindi lazima kesho, Maji Maji watakufa watake wasitake”.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo, Manara amewataka mashabiki na wapenzi wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi kesho kuisapoti timu yao.
  “Nichukue nafasi hii kuwaomba wana Simba wajitokeze kwa wingi kesho katika mchezo wetu na Maji Maji, kwani tuna matumaini makubwa ya kuendeleza wimbi la ushindi,”alisema Manara.
  Kiungo Mwinyi Kazimoto Mwitula anatarajiwa kurejea kwenye mchezo wa kesho baada ya kukosekana katika mchezo uliopita wakishinda 1-0 dhidi ya Azam FC kutokana na kuwa majeruhi.
  Mshambuliaji Ibrahim Hajib aliyetiliwa shaka ya maumivu yuko vizuri na anaweza kucheza pia kesho.
  Kwa ujumla Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa timu zote kuingia viwanjani kusaka pointi.  
  JKT Ruvu Stars wanatarajiwa kuwa wenyeji wa Mbeya City Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani, Ndanda wanatarajiwa kuwa wenyeji wa Azam FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara, Prisons wataikaribisha Mwadui FC Uwanja wa Sokoine, Mbeya na Mtibwa Sugar watakuwa wenyeji wa Mbao FC Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro.
  Ligi Kuu itaendelea Jumapili, Ruvu Shooting wakiikaribisha Toto Africans Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani, Stand United wakimenyana na Yanga SC Uwanja wa Kambarage, Shinyanga na African Lyon wakiwa wenyeji wa Kagera Sugar Uwanja wa Taifa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAWAAMBIA MAJIMAJI KIFO LAZIMA TU KESHO WATAKE WASITAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top