• HABARI MPYA

  Jumapili, Septemba 25, 2016

  NI ZAMALEK NA MAMELODI FAINALI LIGI YA MABINGWA 2016

  TIMU ya Zamalek itamenyana na Mamelodi Sundowns katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2016 licha ya kuchapwa mabaoi 5-2 jana na Wydad Casablanca mjini Rabat, Moroccoo.
  Wababe hao wa Misri wanaingia fainali kwa ushindi wa jumla wa 6-5, baada ya awali kushinda 4-0 katika mchezo wa kwanza nyumbani.
  Iliwachukua dakika 19 tu jana, Wydad kupata mabao mawili ya mwanzo yaliyofungwa na William Jebor na Ismail El Haddad.
  Zamalek wakazidi kujikuta katika wakati mgumu baada ya kuruhusu bao la tatu dakika ya 36 lililofungwa na Bassin Morsi.
  Wydad wakafanikiwa kupata bao la nne dakika ya 45 kupitia kwa Mliberia, Jebor, lakini mabao mawili ya haraka ya Fabrice N'Guessi Ondama yaliirudisha mchezoni Zamalek, kabla ya mshambuliaji Mnigeria, Stanley Nka Ohawuchi kuwafungia wenyeji.
  Mchezo mwingine jana, Mamelodi Sundowns ilishinda 2-0 dhidi ya Zesco United Uwanja wa Lucas Moripe mjini Johannesburg, Afrika Kusini na kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-2 baada ya kufungwa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza mjini Ndola, Zambia.
  Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika itafanyika wikiendi ya Oktoba 14 na 16 kwa mchezo wa kwanza na marudiano Oktoba 21 na 23.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NI ZAMALEK NA MAMELODI FAINALI LIGI YA MABINGWA 2016 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top