• HABARI MPYA

  Jumapili, Septemba 25, 2016

  MAZEMBE WATINGA FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO

  TIMU ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imefanikiwa kwenda fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya sare ya 0-0 na Etoile du Sahel ya Tunisia leo mjini Lubumbashi.
  Kwa sare hiyo ya leo kwenye mchezo wa marudiano, Mazembe inakwenda fainali kwa faida ya bao la ugenini, baada ya kutoa sare ya 1-1 ugenini katika mchezo wa kwanza.
  Mazembe yenye mshambuliaji Mtanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu sasa itakutana na mshindi kati ya FUS Rabat ya Morocco MO Bejaia ya Algeria zinazomenyana mjini Rabat usiku huu katika mchezo wa marudiano.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAZEMBE WATINGA FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top