• HABARI MPYA

  Jumanne, Septemba 27, 2016

  HAJIB AINUKA, AANZA KUJIFUA SIMBA SC

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI tegemeo wa Simba, Ibrahim Hajib Migomba ameanza mazoezi jana kujiandaa na mchezo dhidi ya mahasimu, Yanga SC Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Hajib alizua hofu Jumamosi kwa mashabiki wa Simba baada ya kutoka uwanjani anachechemea dakika ya 21 kufuatia kuumia katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Wekundu wa Msimbazi wakishinda 4-0 dhidi ya Maji Maji ya Songea Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Ibrahim Hajib Migomba ameanza mazoezi jana kujiandaa na mchezo dhidi ya mahasimu, Yanga SC Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

  Hajib alimpisha kiungo Said Hamisi Ndemla, Simba ikiwa inaongoza 1-0 kwa bao Jamal Simba Mnyate – lakini baadaye mchezaji huyo aliyesajilia msimu huu kutoka Mwadui FC ya Shinyanga akaogeza bao moja na Shizza Ramadhani Kichuya akafunga mawili.
  Simba ikaingia kambini jana mjini Morogoro kujiandaa na mchezo dhidi ya Yanga Jumamosi na bahati nzuri, Hajib ameanza maazoezi mepesi jana hiyo hiyo.
  Kocha Mcameroon wa Simba SC, Joseph Marius Omog ataendelea kufuatilia hali ya Hajib hadi keshokutwa kabla ya kuamua rasmi kuhsu hatiam yake kwenye mchezo wa Jumamosi kama atacheza au la.
  Habari njema zaidi kwa Omog ni kwamba mshambuliaji aliyesajiliwa kwa mkopo kutoka Azam FC, Ame Ally naye yupo vizuri kuelekea mchezo wa Jumamosi. 
  Ame alitokea benchi kipindi cha pili katika mchezo dhiri ya Maji Maji na japokuwa hakufunga, lakini alicheza vizuri.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: HAJIB AINUKA, AANZA KUJIFUA SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top