• HABARI MPYA

  Jumatano, Septemba 21, 2016

  TFF WAITUMIA NDEGE KILIMANJARO QUEENS WAPANDIE BUKOBA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeitumia ndege Bukoba timu ya wanawake ya Bara, Kilimanjaro Queens baada ya kusafiri kutoka kwa basi kutoka Jinja, Uganda ambako jana walitwaa CECAFA Challenge  kwa kuifunga Kenya mabao 2-1 Uwanja wa Ufundi, Jinja nchini Uganda.
  Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas amesema kwamba Kili Queens imelazimika kupitia Bukoba ambako ilipiga kambi kabla ya kwenda Jinja ili kusema ahsante kwa wenyeji, lakini pia kuwapa pole ya janga la Tetemeko la Ardhi wakazi lililotokea katika mikoa huo na mikoa jirani ya Kanda ya Ziwa na nchi jirani. 
  Mikoa ambayo iliathirika zaidi ni Kagera na Mwanza kadhalika nchi jirani za Uganda na Rwanda.
  Safari ya ubingwa wa Kilimanjaro Queens ulianzia hatua ya makundi kwa kuilaza Rwanda manbao 3-2 kabla ya kutoka sare tasa na Ethiopia ambayo pia ilivuna ushindi wa mabao 3-2 kutoka kwa Rwanda. Tanzania na Ethiopia zilitoka sare na kurusha sarafu ambako Tanzania ikawa ya kwanza katika kundi B hivyo kucheza na Uganda ambayo ililala kwa mabao 4-0 katika mchezo wa nusu fainali. Na leo Septemba 20, 2016 ikatawazwa kuwa mabingwa kwa ushindi wa mabao 2-1.
  Timu zote shiriki zilikuwa Tanzania, Burundi, Zanzibar, Kenya, Ethiopia, Rwanda pamoja na mwenyeji Uganda. Mashindano ya Kombe la Chalenji la CECAFA kwa timu za wanawake yamefanyika kwa mara ya kwanza jambo linaloleta tafsiri kuwa michuano hiyo inaweza kuinua soka la wanawake kwa ukanda wa nchi za Afrika Mashariki na Kati.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TFF WAITUMIA NDEGE KILIMANJARO QUEENS WAPANDIE BUKOBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top