• HABARI MPYA

    Wednesday, September 21, 2016

    KILIMANJARO QUEENS WAREJEA KWA MSOTO WA BASI NA KOMBE LAO

    Na Mwandishi Wetu, JINJA
    PAMOJA na kuiletea heshima nchi jana kwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kenya jioni ya jana Uwanja wa Ufundi, Jinja, timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Queens iko njiani inarejea nchini kwa basi.
    Kilimanjaro Queens wameondoka mapema tu alfajiri ya leo Jinja kurejea nyumbani Tanzania kwa basi wakipitia Bukoba baada ya kazi nzuri waliyoifanya katika wiki zao mbili zao Uganda.
    Ikumbukwe Queens waliondoka pia kwa basi kwenda Uganda kushiriki mashindano hayo, wakipitia Bukoba pia ambako walicheza mchezo mmoja wa kirafiki dhidi ya Burundi.
    Shukraani kwao, wafungaji wa mabao ya jana katika fainali, Mwanahamisi Omar ‘Gaucho’ na Stumai Abdallah dhidi ya moja la Kenya, lililofungwa na Christine Nafula.


    Kikosi cha Kilimanjaro Queens jana Uwanja wa Ufundi, Jinja, Uganda

    Awali, Tanzania Bara iliongoza Kundi B baada ya kushinda kura ya sarafu kufuatia sare ya 0-0 na Ethiopia katika mchezo wa mwisho wa kundi hilo, hivyo kufungana nayo kwa pointi na wasatani wa mabao kileleni. 
    Kilimanjaro Queens ilianza vizuri michuano hiyo kwa kuibamiza 3-2 Rwanda, mabao yake yakifungwa na Asha Rashid ‘Mwalala’ dakika za 11 na 65 na Stumai Abdallah dakika ya 28, wakati ya wapinzani wao yalifungwa na Ibangarrue Marie na Amina Ally wa Tanzania Bara aliyejifunga.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KILIMANJARO QUEENS WAREJEA KWA MSOTO WA BASI NA KOMBE LAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top