Na Asha Said, DAR ES SALAAM
TIMU ya Friends Rangers ‘Wakombozi wa Manzese’ imeendelea vyema na mbio zake za kuinyemelea Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya jioni hii kuilaza bao 1-0 African Lyon, zote za Dar es Salaam.
Katika mchezo huo wa Ligi Daraja la Kwanza Bara uliofanyika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, bao hilo pekee la Rangers inayomilikiwa na Heri Mzozo na ‘wananchi’ wa Manzese, lilifungwa na Almasi Mkinda kwa penalti dakika ya 18, kufuatia mchezaji wa Lyon kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.
Matokeo hayo, yanaifanya Rangers itimize pointi sita, baada ya awali kuifunga 2-1 Lipuli ya Iringa kwenye Uwanja huo huo, Karume.

0 comments:
Post a Comment