• HABARI MPYA

    Wednesday, October 15, 2014

    UGANDA MGUU NJE MBIO ZA AFCON 2015…DRC YAITANDIKA 4-3 IVORY COAST KWAO ABIDJAN NA YAYA TOURE WAO

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    UGANDA imezidi kujipunguzia matumaini ya kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani nchini Morocco, baada ya kuchapwa bao 1-0 na Togo katika mchezo wa Kundi E jioni ya leo.
    Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Kague mjini Lome, bao lililoizamisha Uganda lilifungwa na Serge Akakpo dakika ya 70 na Togo sasa inapanda nafasi ya pili kwa pointi sita ilizovuna kwa timu ya Milutin Sredojevich ‘Micho’ ndani ya siku tano. Uganda inabaki na pointi nne katika nafasi ya tatu, wakati Ghana imejiimarisha kileleni mwa kundi hilo, kufuatia ushindi wa 3-1 Guinea Uwanja wa Tamale mjini Tamale.
    Mabao ya Ghana yamefungwa na Asamoah Gyan dakika ya 16, Andrew Ayew kwa penalti dakika ya 58 na Agyemang-Badu dakika ya 90, wakati la Guinea limefungwa na Mohamed Yattara dakika ya 35.
    Katika Kundi A, Nigeria imeilaza 3-1 Sudan Uwanja wa Taifa wa Abuja, mabao ya Ahmed Musa dakika ya 48 na 90 na Aaron Olanare dakika ya 66, huku bao pekee la wapinzani wao likifungwa na Salah Ibrahim dakika ya 56.

    Kundi F, Zambia imeifunga 3-0 Niger Uwanja wa Taifa wa Mashujaa mjini Lusaka mabao ya Rainford Kalaba dakika ya 58, Emmanuel Mayuka dakika ya 73 na kipa Kennedy Mweene kwa penalti dakika ya 87.  
    Cameroon imeshinda mabao 2-0 dhidi ya Sierra Leone mabao ya Leonard Kweuke dakika ya nne na Stephane Mbia dakika ya saba Uwanja wa 
    Ahmadu Ahidjo mjini Yaounde.
    Misri imeifunga 2-0 Botswana mchezo wa Kundi G, mabao ya Amr Gamal dakika ya 52 na Mohamed Salah dakika ya 72, wakati mchezo mwingine wa kundi hilo kati ya Senegal na Tunisia unaendelea.
    Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imewafunga 4-3 wenyeji Ivory Coast mchezo wa Kundi D, mabao ya DRC yamefungwa na Neeskens Keban dakika ya 21, Junior Kabananga dakika ya 35 na Jeremy Bokila dakika ya 36 na 89, wakati mabao ya Ivory Coast iliyompoteza Yannick Kessie aliyetolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 47, yamefungwa na Yaya Toure dakika ya 25 na Solomon Kalou dakika ya 69 na 72.    
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UGANDA MGUU NJE MBIO ZA AFCON 2015…DRC YAITANDIKA 4-3 IVORY COAST KWAO ABIDJAN NA YAYA TOURE WAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top