• HABARI MPYA

    Wednesday, October 15, 2014

    CAMEROON YABISHA HODI MOROCCO 2015...YAIFUMUA 2-0 SIERRA LEONE

    CAMEROON imejiongezea matumaini ya kupata nafasi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2014, kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Sierra Leone jioni ya leo.
    Shukrani kwao, Leonard Kweuke aliyefunga dakika ya nne na Stephane Mbia dakika ya saba Uwanja wa 
    Ahmadu Ahidjo mjini Yaounde.
    Cameroon sasa inatimiza pointi 10, ikifuatiwa na Ivory Cost yenye pointi sita kabla ya matokeo ya mchezo wake na DRC jioni ya leo.
    Hali mbaya kwa Sierra Leone ambayo baada ya mechi nne inabaki na pointi moja. Timu mbili kila kundi zitajipatia tiketi ya kwenda Morocco mapema mwakani.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CAMEROON YABISHA HODI MOROCCO 2015...YAIFUMUA 2-0 SIERRA LEONE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top