• HABARI MPYA

    Tuesday, October 14, 2014

    RANGERS KUMENYANA NA AFRICAN LYON DARAJA LA KWANZA KESHO KARUME

    Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KIKOSI cha timu ya Friends Rangers, yenye makazi yake Magomeni Kagera Dar es Salaam, kesho kinashuka kwenye Uwanja wa Karume,
    Dar es Salaam, kuvaana na timu ya African Lyon, katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara.
    Timu hizo zinacheza mecho wao wa pili huku Rangers ikiingia dimbani na pointi tatu za mchezo wake wa kwanza, baada ya kuifunga Lipuli ya Iringa kwa mabao 2-1.
    Kocha wa Friends Rangers, Ally Yussuf 'Tigana' kushoto na Mbunge wa Kinondoni, Iddi Azzan

    Ofisa Habari wa timu hiyo Friends Rangers, Asha Kigundula, amesema wamejipanga vizuri kushinda mchezo huo wa pili licha ya kutambua katika mechi kuna matokeo ya aina tatu.
    Kigundula alisema kikosi chao chini ya kocha wao Mkuu, Ally Yussuf ‘Tigana’, kinawaomba wapenzi wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao.
    "Nina amini hakuna matokeo mazuri kama kuwa kitu kimoja hivyo wakazi wote wa Kagera, Mwembe Chai, Manzese, Ubungo na Magomeni tunaomba mshikamano wenu, mjitokeze kuishangilia timu yetu ambayo tayari imeanza vizuri kwa kushinda mchezo wa kwanza"alisema Kigundula
    Alisema kuwa kila mchezaji ana hali kubwa ya kushinda mchezo huo ili ijiweke vizuri.
    Kigundula alisema wamejipanga kushinda mechi zao za ndani na nje ya Mkoa wa Dar es Salaam, ili waweze kupanda msimu ujao waweze kucheza Ligi Kuu msimu ujao wa mwaka 2015/16.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RANGERS KUMENYANA NA AFRICAN LYON DARAJA LA KWANZA KESHO KARUME Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top