Na Ameir Khalid, DAR ES SALAAM
KUNA kila dalili kwamba mashindano ya kuwania Kombe la Mapinduzi mwakani yatakosa msisimko unaotarajiwa.
Hali hiyo huenda ikajitokeza kutokana na kuwepo uwezekano kwa timu mashuhuri nchini, Simba SC, Yanga SC, Azam FC na nyengine za Tanzania Bara kutoweza kushiriki michuano hiyo inayofanyika kila mwezi Januari ikiwa sehemu ya maadhimisho ya sherehe za Mapinduzi ya Januari 12, 1964.
Uchunguzi wetu umegundua kwamba katika kalenda yake na ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2014/2015, Shirikisho la Soka Tanzania Bara halikuyatambua mashindano hayo, kwani wakati yakiendelea, ligi hiyo itakuwa ikivinjari huku klabu zote hizo zikikabiliwa na mechi katika viwanja mbalimbali.
Kwa kawaida, mashindano hayo ambayo mwakani yatafanyika kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar, huanza Januari 2 hadi 12, ambayo ni siku ya kilele cha maadhimisho hayo.
Mbali na klabu hizo kubwa nchini, katika miaka ya karibuni, michuano hiyo imeongezewa ladha kwa kuzialika pia timu kutoka nchi jirani za Kenya na Uganda.
Katika kuiangalia kwa kina ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Zanzibar Leo limebaini kuwa, TFF imeyatambua mashindano kadhaa ya taifa, kikanda na Afrika, ambapo tarehe zake zinaonesha kuwa ligi hiyo ama itakuwa imesimama au imeziruka mechi za klabu zitakazoshiriki michuano hiyo ya kimataifa.
Michuano hiyo ni ile ya Chalenji inayotarajiwa kuanza Novemba 20 jijini Addis Ababa nchini Ethiopia na kuchukua wiki mbili, ‘Uhai Cup’ inayoshirikisha timu za chini ya miaka 20 za klabu za Ligi Kuu, pamoja na Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika (CAF).
Ratiba hiyo ya TFF inaonesha kuwa, mzunguko wa kumi ya Ligi Kuu hiyo utaanza Disemba 20 na kuendelea hadi mzunguko wa 17 ambao utamalizika Februari 8, 2015, bila kuonesha kwamba mechi za Simba, Yanga na Azam zitasimama kupisha mashindano ya Kombe la Mapinduzi.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, Januari 1, 2015 Simba na Azam zitapambana uwanja wa Taifa Dar es Salaam, wakati Januari 3, Yanga itakuwa uwanja wa Jamhuri Morogoro kuwavaa maafande wa Polisi.
Aidha, Januari 10, wekundu wa Msimbazi Simba, wataikaribisha JKT Ruvu uwanja wa Taifa Dar es Salaam, huku Azam wakiwa wageni wa Mgambo JKT katika dimba la Mkwakwani Tanga, na Januari 11 Yanga itacheza na Ndanda FC uwanja wa Taifa.
Siku zote hizo, mashindano ya Kombe la Mapinduzi yatakuwa yanaendelea mjini Zanzibar.
Wakati ikiwa imebakia miezi miwili na nusu kabla kuanza kwa mashindano ya Kombe la Mapinduzi, bado kamati inayosimamia ngarambe hizo iliyoko chini ya ulezi wa Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi, haijakutana kupanga maandalizi.

![]() |
| Kipa wa Simba SC, Ivo Mapunda akipokea Kombe la ushindi wa pili wa Mapinduzi mwaka huu |

.png)
0 comments:
Post a Comment