• HABARI MPYA

    Sunday, October 19, 2014

    MESSI NA NEYMAR WOTE WAFUNGA BARCA IKIUA 3-0 LA LIGA NA KUPAA ZAIDI KILELENI

    BARCELONA imeshinda mechi yake ya saba kati ya nane za mwanzo za La Liga msimu huu, kufuatia kuilaza mabao 3-0 Eibar usiku wa jana.
    Shukrani kwao wafungaji wa mabao hayo, Xavi dakika ya 60, Neymar dakika ya 72 na Lionel Messi dakika ya 75.
    Kikosi cha Luis Enrique sasa kimecheza mechi nane bila ya kuruhusu nyavu zake kuguswa, kikiwazidi kwa pointi nne wapinzani wao, Real Madrid kileleni mwa La Liga. 
    Kikosi cha Barcelona kilikuwa: Bravo, Alves, Pique, Mathieu, Alba, Mascherano, Sergi Roberto/Iniesta dk55, Xavi, Pedro/Sandro dk71, Messi na Neymar/Munir dk76.
    Eibar: Irureta, Lillo, Ekisa, Boveda, Albentosa, Abraham, Errasti, Dani Garcia, Javi Lara, Capa/Boateng dk75 na Saul Berjon/Nieto dk76.
    Messi kulia na Neymar wakipongezana jana
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MESSI NA NEYMAR WOTE WAFUNGA BARCA IKIUA 3-0 LA LIGA NA KUPAA ZAIDI KILELENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top