• HABARI MPYA

    Tuesday, October 14, 2014

    MESSI APIGA MBILI ARGENTINA IKIICHAPA 7-0 HONG KONG

    ARGENTINA imeifunga mabao 7-0 Hong Kong katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliomalizika hivi kaibuni.
    Mabao ya Argentina yamefungwa na Ever Banega dakika ya 19, Gonzalo Higuain mawili dakika ya 43 na 54 sawa na Nicolas Gaitan dakika ya 45 na 72 na Lionel Messi dakika ya 66 na 85.
    Katika mchezo huo, ambao Lionel Messi na Angel di Maria walianzia benchi, Argentina ilizinduka baada ya kutoka kuchapwa 2-0 na wapinzani wao wakubwa, Brazil.
    Kikosi cha Argentina kilichoanza; Guzman, Roncaglia, Otamendi, Vergini, Vangioni, Perez, Gago, Banega, Pastore, Higuain na Gaitan
    Hong Kong; Yapp, C. Lee, Agbo, Naegelein, Huang, Xu, W. Lee, Cheung, Chan, Karikari na Ju.
    Messi amefunga mabao mawili katika ushindi wa 7-0 wa Argentina dhidi ya Hong Kong leo
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MESSI APIGA MBILI ARGENTINA IKIICHAPA 7-0 HONG KONG Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top