NYOTA wa Manchester United, Angel di Maria alitaka fedha nyingi ili abaki Real Madrid, kwa mujibu wa kocha Carlo Ancelotti.
Kocha huyo wa Bernabeu amesema klabu iligoma kuvunja utaratibu wake wa ulipaji mishahara ili kumbakiza Muargentina huyo, ambaye amehamia Old Trafford kwa dau la uhamisho la Pauni Milioni 60 msimu huu.
Di Maria ameingia vizuri kwenye kikosi cha Louis van Gaal hadi sasa akiwa amefunga mabao matatu katika mechi tano za Ligi Kuu ya England.
Angel di Maria amejiunga na Manchester United kutoka Real Madrid msimu huu kwa dau la rekodi Uingereza la Pauni Milioni 60
Carlo Ancelotti amesema wing huyo wa Argentine amekwenda England kufuata 'mahela' mengi
Lakini bosi huyo wa Real, Ancelotti anaamini sera za klabu zilikuwa ni bora zaidi kuliko kumbakiza Di Maria kwenye safu ya ushambuliaji ambayo tayari inao Cristiano Ronaldo, Gareth Bale na James Rodriguez.
"Nilikubaliana na klabu. Kuna wakati ambao klabu inabidi iseme hapana. Huwezi kubadilisha sera za klabu kwa sababu ya mchezaji mmoja. Di Maria alitaka fedha nyingi na akaona ni bora kuondoka kuzifuata. Klabu isingeweza kumpa fedha alizotaka,"amesema Ancelotti.
0 comments:
Post a Comment