Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi amesema utaratibu wa kukata asilimia tano ya pato la mikataba ya udhamini wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uko pale pale.
Pamoja na hayo, Rais Malinzi ameitaka Bodi ya Ligi kuhakikishia inasimamia ukusanywaji wa fedha hizo mara moja. Ligi Kuu inadhaminiwa na Vodacom wakati pia imeiuzia haki za matangazo ya Televisheni, kampuni ya Azam Media Limited.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mchana wa leo, makao makuu ya TFF, Dar es Salaam- Malinzi amesema kwamba Bodi ya Ligi haina mamlaka ya kupinga maamuzi yoyote ya Kamati ya Utendaji.
Amesema chombo pekee chenye uwezo wa kupinga maamuzi ya Kamati ya Utendaji ya TFF ni Mkutano Mkuu pekee na si vinginevyo.
Malinzi amesema fedha hizo zinatarajiwa kuingia kwenye mfuko maalum wa maendeleo ya vijana ulioundwa na Kamati yake ya Utendaji, chini ya Mwenyekiti, Leodegar Tenga ambaye ni rais wa zamani wa TFF.
Amesema Mfuko huo utasimamia timu mbili za vijana chini ya umri wa miaka 12 itakayoanza kuandaliwa mara moja kwa ajili ya Fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa 17 mwaka 2019, ambazo Tanzania wameomba uenyeji pamoja na U14 ambayo itawania tiketi ya Fainali za U17 mwaka 2017 nchini Madagascar.
“Hizi timu zitaundwa mara moja na kuingia kambini, U12 watakwenda shule ya Alliance Academy (Mwanza) na wale U14 watakwenda shule ya Lord Burden (Bagamoyo) ambako watakuwa wanasoma na kufanya mazoezi kuandaliwa kwa michuano,”amesema
Kuhusu ‘mikwara’ ya eti klabu zitaenda mahakamani iwapo TFF itakata asilimia tano kwenye pato lao, Malinzi amesema Bodi ya Ligi Kuu ipo chini ya utaratibu.
“Bodi ya Ligi Kuu ina vikao vyake halali kwa mujibu wa utaratibu, wanatakiwa wafuate utaratibu huo katika. Lakini pia nataka niseme, Bodi ya Ligi haijasaini Mkataba wowote wa udhamini, mikataba yote imesainiwa baina ya wadhamini na TFF,”amesema.
Hata hivyo, Malinzi amesema wakati wa upitishwaji wa kanuni hiyo ya kukata asilimia tano kwenye pato la wadhamini wa Ligi Kuu, viongozi wa Bodi ya Ligi- Mwenyekiti Hamad Yahya na Makamu wake, Sheikh Said Muhammad pamoja na Mtendaji wa kuajiriwa, Silas Mwakibinga walikuwepo.

![]() |
Rais wa TFF, Jamal Malinzi kushoto akizungumza na Waandishi wa Habari leo makao makuu ya TFF. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Wanachama wa shirikisho hilo, Eliud Mvella |
Amesema chombo pekee chenye uwezo wa kupinga maamuzi ya Kamati ya Utendaji ya TFF ni Mkutano Mkuu pekee na si vinginevyo.
Malinzi amesema fedha hizo zinatarajiwa kuingia kwenye mfuko maalum wa maendeleo ya vijana ulioundwa na Kamati yake ya Utendaji, chini ya Mwenyekiti, Leodegar Tenga ambaye ni rais wa zamani wa TFF.
Amesema Mfuko huo utasimamia timu mbili za vijana chini ya umri wa miaka 12 itakayoanza kuandaliwa mara moja kwa ajili ya Fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa 17 mwaka 2019, ambazo Tanzania wameomba uenyeji pamoja na U14 ambayo itawania tiketi ya Fainali za U17 mwaka 2017 nchini Madagascar.
“Hizi timu zitaundwa mara moja na kuingia kambini, U12 watakwenda shule ya Alliance Academy (Mwanza) na wale U14 watakwenda shule ya Lord Burden (Bagamoyo) ambako watakuwa wanasoma na kufanya mazoezi kuandaliwa kwa michuano,”amesema
Kuhusu ‘mikwara’ ya eti klabu zitaenda mahakamani iwapo TFF itakata asilimia tano kwenye pato lao, Malinzi amesema Bodi ya Ligi Kuu ipo chini ya utaratibu.
“Bodi ya Ligi Kuu ina vikao vyake halali kwa mujibu wa utaratibu, wanatakiwa wafuate utaratibu huo katika. Lakini pia nataka niseme, Bodi ya Ligi haijasaini Mkataba wowote wa udhamini, mikataba yote imesainiwa baina ya wadhamini na TFF,”amesema.
Hata hivyo, Malinzi amesema wakati wa upitishwaji wa kanuni hiyo ya kukata asilimia tano kwenye pato la wadhamini wa Ligi Kuu, viongozi wa Bodi ya Ligi- Mwenyekiti Hamad Yahya na Makamu wake, Sheikh Said Muhammad pamoja na Mtendaji wa kuajiriwa, Silas Mwakibinga walikuwepo.
0 comments:
Post a Comment