• HABARI MPYA

    Saturday, October 18, 2014

    AZAM YAIKANDAMIZA MBEYA CITY 1-0 SOKOINE NA KUPAA KILELENI LIGI KUU

    Na Mahmoud Zubeiry, MBEYA
    MABINGWA watetezi, Azam FC wameilaza bao 1-0 Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni hii Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
    Shukrani kwake, beki Aggrey Morris akiyefunga bao hilo pekee dakika ya 19 kwa shuti kali la mpira wa adhabu kutoka umbali wa miya 20, kufuatia Didier Kavumbangu kuangushwa na Yohanna Morris wa Mbeya City.
    Ushindi huo, unaifanya Azam FC itimize pointi 10, baada ya mechi nne na kupanda kileleni kwa wastani wa mabao, baada ya Mtibwa Sugar kulazimishwa sare ya bila kufungana na Polisi mjini Morogoro. Mbeya City inabaki na pointi zake tano za mechi nne pia.
    Wachezaji wa Azam wakishangilia bao lao leo Sokoine. Aggrey wa tatu kulia 

    Mwagane Yeya wa Mbeya City kulia akimkata 'mtama' kiungo wa Azam FC, Kipre Balou leo
    Hii ni mara ya pili mfululizo, Azam FC inaifunga Mbeya City kwenye Uwanja huu, baada ya Aprili 13 mwaka huu kuichapa pia mabao 2-1 katika mchezo wa mzunguko wa pili wa ligi hiyo.
    Kipa Aishi Manula leo alikuwa shujaa upande wa Azam FC kutokana na kuokoa michomo mingi ya hatari.
    Kikosi cha Mbeya City kilikuwa; David Burhan, Deogratius Julius, Hassan Mwasapili, Yussuf Abdallah, Yohana Morris, Anthony Matogolo, Saad Kipanga/Peter Mwalyanzi, Steven Mazanda, Paul Nonga, Mwagane Yeya na Deus Kaseke.
    Azam FC; Aishi Manula, Shomary Kapombe, Gardiel Mbaga, Said Mourad, Aggrey Morris, Kipre Balou, Himid Mao, Erasto Nyoni, Didier Kavumbangu/Gaudence Mwaikimba, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na Kipre Tchetche/Mudathir Yahya. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM YAIKANDAMIZA MBEYA CITY 1-0 SOKOINE NA KUPAA KILELENI LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top