KLABU ya Southampton imesajili wachezaji wawili, Shane Long kwa Pauni Milioni 12 kutoka Hull City na Florin Gardos kutoka Steaua Bucharest ya Romania.
Long, mwanasoka wa kimataifa wa Jamhuri ya Ireland na Mromania Gardos wanafanya jumla ya wachezaji wapya saba kusajiliwa St Mary na kocha Ronald Koeman.
Koeman tayari amewanunua Ryan Bertrand, Fraser Forster, Graziano Pelle, Dusan Tadic na Saphir Taider katika jitihada za kukisuka upya kikosi chake baada ya kuuza wachezaji kadhaa.
Kwa upande wake, Gardos mwenye umri wa miaka 25, amesaini mkataba wa miaka mine kutoka kwa mabingwa wa Romania, Steaua Bucharest.
Na akimzungumzia mchezaji huyo kwenye tovuti ya klabu hiyo, kocha Koeman alisema: "Nimefurahi sana kumpata Florin hapa,".
Florin Gardos amesaini Mkataba wa miaka minne
0 comments:
Post a Comment