• HABARI MPYA

    Wednesday, August 13, 2014

    MSIBA MWINGINE YANGA SC, KATIBU WA ZAMANI AFARIKI DUNIA LEO, ATAZIKWA KESHO MAGOMENI

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    YANGA SC imepata msiba mwingine ndani ya mbili tu, baada ya aliyekuwa Katibu wake wa zamani, Ally Bwamkuu kufariki dunia asubuhi ya leo nyumbani kwake, Kongowe mwisho mjini Dar es Salaam.
    Jana Yanga SC ilimpoteza aliyekuwa dereva wa basi la wachezaji, Maulid Kiula aliyefariki nyumbani kwake, Ilala, Dar es Dalaam ambaye alitarajiwa kuzikwa leo.
    Pumzika kwa amani; Ally Bwamkuu enzi za uhai wake

    Taarifa zilizothibitishwa na Meneja wa Yanga SC, Hafidh Saleh zimesema kwamba, Bwamkuu ambaye alishika nyadhifa nyingine mbalimbali ndani ya klabu hiyo tangu miaka ya 1980 atazikwa kesho makaburi ya Mwinyimkuu, Magomeni, Dar es Salaam.
    “Ni kweli, Bwamkuu hatunaye. Ila Katibu (Benno Njovu) anaendelea kuwasiliana kwa familia ya marehemu kwa taarifa zaidi, na baada ya hapo nadhani klabu itatoa muongozo kwa wanachama na wapenzi juu ya namna ya kushirki msiba huo,”amesema Hafidh. 
    Mbali na kuongoza Yanga SC, Bwamkuu pia ameshika nyadhifa mbalimbali katika bodi za soka, tangu enzi za FAT na sasa TFF na amewahi kuwamo katika Kamati ya Saidia Taifa Stars ishinde, upande. Mungu ampumzishe kwa amani marehemu. Amin.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MSIBA MWINGINE YANGA SC, KATIBU WA ZAMANI AFARIKI DUNIA LEO, ATAZIKWA KESHO MAGOMENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top