• HABARI MPYA

    Thursday, February 06, 2014

    WAWAKILISHI WA CAVANI WATUA LONDON, HUENDA AKAENDA MAN UNITED AU CHELSEA

    WAWAKILISHI wa Edinson Cavani wamewasili London leo wakati mshambuliaji huyo anatazamiwa kuondoka Paris Saint-Germain. 
    Mshambuliaji huyo wa Uruguay yupo nje kwa sababu ya majeruhi, ambayo yatamuweka nje kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi Bayer Leverkusen. 
    Amekuwa na mafanikio Ufaransa, lakini inafahamika mustakabali wake haueleweki kwenye klabu hiyo, kwa sababu hafurahii kuchezeshwa pembeni ya Zlatan Ibrahimovic. 
    Msukumo wa kuondoka: Edinson Cavani anavutiwa na Ligi Kuu ya England na Chelsea na Manchester United zinamuhitaji
    Big hit: Cavani has been a success since joining PSG from Serie A outfit Napoli in a £54m transfer
    Mkali: Cavani amekuwa na mafanikio tangu ajiunge na PSG kutoka vigogo wa Serie A, Napoli kwa Pauni Milioni 54

    BIN ZUBEIRY inafahamu Manchester United imewahia kutaka kumsajii Cavani wakati wa kocha wa zamani, Sir Alex Ferguson aliyewahi kuwasiliana na beki wa zamani wa timu yake ya Old Trafford, Laurent Blanc kuangalia uwezekano wa kuwauzia mchezaji huyo mwezi uliopita. 
    United inabakia kuwa katika nafasi nzuri ya kumsaili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, lakini sasa Chelsea nayo imeingia vitani kuwania saini yake. 
    Klabu zote zinagongana pia kwa wachezaji wengine na tayari kocha Jose Mourinho amepiga hatua katika kuwania saini za nyota wa Atletico Madrid, Diego Costa  na Mario Mandzukic wa Bayern Munich. 
    Two's company: Cavani has been used in a wider role beside PSG's Swedish striker Zlatan Ibrahimovic
    Wawili washirika: Cavani amekuwa akitumia pembeni pembeni ya mshambuliaji wa kwanza wa PSG, Msweden striker Zlatan Ibrahimovic

    Bei ya kuuzwa Cavani haijatajwa. lakini PSG itataka dau sawa na ililotoa kumnunua kutoka Napoli msimu huu, Pauni Milioni 54
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WAWAKILISHI WA CAVANI WATUA LONDON, HUENDA AKAENDA MAN UNITED AU CHELSEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top