• HABARI MPYA

    Friday, February 07, 2014

    VIDIC AWAAGA MAN UNITED, ASEMA; "NAONDOKA MSIMU UKIISHA"

    BEKI wa Manchester United, Nemanja Vidic ametangaza kuondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu baada ya kukataa kuongeza Mkataba.
    Kocha David Moyes alikuwa tayari kumbakiza Nahodha wake huyo Old Trafford, lakini Vidic, anayemaliza Mkataba mwishoni mwa msimu, ameamua kuondoka baada ya kuitumikia Manchester kwa miaka minane.
    Mserbia huyo ameshinda mataji 15 tangu awasili klabu hiyo akitokea Spartak Moscow ya Urusi kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 7, Januari mwaka 2006, na baadayekuwa Nahodha chini ya kocha Sir Alex Ferguson.
    Katika taarifa yake, Vidic amesema: "Ni mwaka wa mwisho wa Mkataba wangu na nimekuwa na miaka minane mizuri hapa.
    Anaondoka: Beki wa United, Vidic (kushoto) ametangaza kuondoka mwishoni mwa msimu
    New boy: Vidic was signed by former United boss Sir Alex Ferguson from Spartak Moscow in January 2006
    Aliposajiliwa: Vidic alisainiwa na kocha wa zamani wa United, Sir Alex Ferguson kutoka Spartak Moscow Januari mwaka 2006
    Big hit: Vidic has made almost 400 appearances for the Red Devils since joining for £7million
    Vidic amaichezea takriban mechi 400 Man United
    All smiles: Vidic lifts the 2010-11 Premier League trophy, United's record-breaking 19th league title
    Tabasamu: Vidic akiinua Kombe la ubingwa wa Ligi Kuu msimu wa 2010-11, taji lililoweka rekodi ya klabu hiyo kutwaa mara nyingi zaidi, mara19

    MATAJI ALIYOSHINDA VIDIC MAN UNITED

    MATAJI YA TIMU:
    Ligi Kuu: 2006/07, 2007/08, 2008/09, 2010/11, 2012/13
    Ligi ya Mabingwa Ulaya: 2007/08
    Kombe la Ligi: 2005/06, 2008/09, 2009/10
    Ngao ya Jamii: 2007, 2008, 2010, 2011, 2013
    Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA: 2008
    TUZO BINAFSI; 
    Mchezaji Bora wa Mwaka wa PFA: 2006/07, 2007/08, 2008/09
    Mchezaji Bora wa Mwaka wa Ligi Kuu Engand; 2008/09, 2010/11
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: VIDIC AWAAGA MAN UNITED, ASEMA; "NAONDOKA MSIMU UKIISHA" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top