Na Prince Akbar, Dar es Salaam
KOCHA wa Yanga, Mholanzi Hans van der Pluijm amesema wachezaji wake wako 'fiti' kwa mechi yao ya kwanza ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya timu ya Komorozine de Domoni kutoka Visiwa vya Comoro itakayopigwa Uwanja, Dar es Salaam wa Taifa kesho.
Komorozine de Domoni ambao ndiyo wawakilishi wa visiwa hivyo katika mashindano hayo makubwa kwa ngazi ya klabu barani Afrika wako nchini tangu juzi kwa ajili ya mechi hiyo na jana walifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam na wanashuka Uwanja wa Taifa kufanya mazoezi yao ya mwisho kabla ya mchezo huo kama kanuni za mashindano zinavyoelekeza.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY kuhusu mechi hiyo baada ya mazoezi ya kikosi cha Yanga kilichopo mafichoni mjini Bagamoyo Pwani leo asubuhi, Pluijm amesema maandalizi ya mchezo huo kwa kikosi chake yamekaliika na vijana wote wako fiti, kiakili na morali yao iko juu hivyo naamini tutaibuka na ushindi.
“Nimekuwa na timu kwa takribani wiki nne sasa tangu niungane na wachezaji nchini Uturuki, maendeleo ni mazuri, upungufu uliojitokeza katika mchezo uliopita dhidi ya Mbeya City tumeufanyia kazi na sasa kikosi kimezidi kuimarika,”amaesema Pluijm.
Yanga ambayo imeweka kambi mjini Bagamoyo kujiandaa na mchezo huo, imekuwa ikifanya mazoezi mara mbili kwa siku kujiandaa na mchezo huo wa hatua ya wali ya mashindano hayo ambao kama watafuzu baada ya kucheza mechi mbili za nyumbani na ugenini ndani ya wiki mbili, watachuana na mabingwa wa Afrika, Al Ahly ya Misri katia hatua ya pili.

![]() |
| Tupo kamili; Kocha wa Yanga SC, Hans van der Pluijm amesema kikosi chake kipo tayari kwa mechi kesho |
Akizungumza na BIN ZUBEIRY kuhusu mechi hiyo baada ya mazoezi ya kikosi cha Yanga kilichopo mafichoni mjini Bagamoyo Pwani leo asubuhi, Pluijm amesema maandalizi ya mchezo huo kwa kikosi chake yamekaliika na vijana wote wako fiti, kiakili na morali yao iko juu hivyo naamini tutaibuka na ushindi.
“Nimekuwa na timu kwa takribani wiki nne sasa tangu niungane na wachezaji nchini Uturuki, maendeleo ni mazuri, upungufu uliojitokeza katika mchezo uliopita dhidi ya Mbeya City tumeufanyia kazi na sasa kikosi kimezidi kuimarika,”amaesema Pluijm.
Yanga ambayo imeweka kambi mjini Bagamoyo kujiandaa na mchezo huo, imekuwa ikifanya mazoezi mara mbili kwa siku kujiandaa na mchezo huo wa hatua ya wali ya mashindano hayo ambao kama watafuzu baada ya kucheza mechi mbili za nyumbani na ugenini ndani ya wiki mbili, watachuana na mabingwa wa Afrika, Al Ahly ya Misri katia hatua ya pili.

.png)
0 comments:
Post a Comment