Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
MSHAMBULIAJI wa klabu ya Yanga SC ya Dar es Salaam, Mrisho Khalfan Ngassa anasumbuliwa na maumivu ya nyama za paja, ingawa anajikongoja hivyo hivyo kufanya mazoezi.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana, Ngassa alisema kwamba aliumia nyama Jumamosi baada ya kufunga bao lake pili kati ya matatu katika ushindi wa 7-0 dhidi ya Komorozine ya Comoro katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini akajitahidi kumalizia mchezo.
“Nilidhamiria kufunga mabao matatu katika mchezo huo, hivyo nikajitahidi sana kuvumilia nimalizie mchezo ili nitimize lengo langu. Na leo (jana) nimefanya mazoezi na wenzangu ila nasikia kama nyama zinauma,”alisema Ngassa.
Hata hivyo, Ngassa amesema kwamba amekwishawasiliana na Daktari wa timu hiyo, Juma Sufiani ambaye ameahidi kumfanyia vipimo leo kabla ya tiba.
Tangu amerejea Yanga SC msimu huu kutoka kwa mahasimu, Simba SC tayari amekwishaichezea timu hiyo mechi 19 na kuifungia mabao 12, yakiwemo saba ya Ligi Kuu, ingawa alikosa mechi sita za awali akitumikia adhabu kwa kosa la kusaini timu ya Jangwani akiwa ana Mkataba na Wekundu wa Msimbazi.

![]() |
| Kijana anaumwa; Mrisho Ngassa anasumbuliwa na maumivu ya nyama na chini akiondoka na mpira baada ya kufunga hat trick dhidi ya Komorozine |
“Nilidhamiria kufunga mabao matatu katika mchezo huo, hivyo nikajitahidi sana kuvumilia nimalizie mchezo ili nitimize lengo langu. Na leo (jana) nimefanya mazoezi na wenzangu ila nasikia kama nyama zinauma,”alisema Ngassa.
Hata hivyo, Ngassa amesema kwamba amekwishawasiliana na Daktari wa timu hiyo, Juma Sufiani ambaye ameahidi kumfanyia vipimo leo kabla ya tiba.
Tangu amerejea Yanga SC msimu huu kutoka kwa mahasimu, Simba SC tayari amekwishaichezea timu hiyo mechi 19 na kuifungia mabao 12, yakiwemo saba ya Ligi Kuu, ingawa alikosa mechi sita za awali akitumikia adhabu kwa kosa la kusaini timu ya Jangwani akiwa ana Mkataba na Wekundu wa Msimbazi.

.png)
0 comments:
Post a Comment