• HABARI MPYA

    Tuesday, February 11, 2014

    MKWE WA KOCHA YANGA SC AINGIA KWENYE ORODHA YA VIBIBI VYA KIHISTORIA TANZANIA

    Na Dina Ismail, Dar es Salaam
    KUFIKISHA umri wa miaka 100 kwa mwanadamu si jambo jepesi, na inapotokea hakika huwa jambo la faraja.
    Mama wa Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Dodoma, Betty Mkwasa na mume wa kocha wa Yanga SC, Charles Boniface Mkwasa amegonga miaka 100 na bado anadunda.
    Mke wa kiungo wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Betty Mkwasa ameandika kwenye ukurasa wake wa facebook kwamba hana hakika kama anaweza kufikia umri wa mama yake mzazi, yeye akiwa mtoto wa saba kuzaliwa na bibi huyo.
    Miaka 100 bado anadunda; Kocha wa Yanga SC, Charles Boniface Mkwasa kulia akiwa na mkewe Betty kushoto na mkwewe katikati ambaye ametimiza miaka 100 

    “I wish ningefika umri wa mama yangu huyu!! Kashuhudia mtoto wake wa saba akisheherekea miaka 25 ya ndoa!!! Hivyo Yeye ana umri gani!? Anagonga 100 hapo!!! Hongera mama!!!,”ameandika Betty, mtangazaji wa zamani wa Redio Tanzania (RTD) na Redio One na ITV. 
    Ikumbukwe hivi karibuni, Betty amesherehekea kutimiza miaka 25 ya ndoa yake na mchezaji wa zamani hodari nchini, aliyegeuka kuwa kocha bora nchini.  

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MKWE WA KOCHA YANGA SC AINGIA KWENYE ORODHA YA VIBIBI VYA KIHISTORIA TANZANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top