BAO la dakika ya 87 la Victor Anichebe limetosha kuipokonya tonge mdomoni Chelsea baada ya West Brom kulazimiha sare ya 1-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
Ivanovic alitangulia kuifungia bao timu ya Jose Mourinho dakika ya 45 na ikaonekana kama the Blues wataondoka na ushindi ugenini, lakini mwisho wa mchezo wakaambulia pointi moja.
Matokeo hayo yanaifanya Chelsea ifikishe pointi 57 baada ya kucheza mechi 26 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi mbili zaidi dhidi ya Arsenal walio katika nafasi ya pili, ambao hata hivyo wamecheza mechi 25.
La kuongoza: Mserbia Ivanovic akishangilia baada ya kuifungia Chelsea bao la kuongoza Uwanja wa Hawthorns



.png)
0 comments:
Post a Comment