• HABARI MPYA

    Monday, February 10, 2014

    KOCHA MARSH ASUBIRI VIPIMO VYA MWISHO

    Na Boniface Wambura, Dar es Salaam 
    KOCHA Msaidizi wa Taifa Stars, Sylvester Marsh ambaye amelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) anasubiri vipimo vya mwisho ili aweze kuanza matibabu.
    Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemtoa kocha huyo nyumbani kwake jijini Mwanza na kumleta Dar es Salaam kwa lengo la kuhakikisha anapata matibabu zaidi na kwa uangalizi wa karibu.
    Kocha Sylvester Marsh katikati

    Tayari majibu ya kipimo cha kwanza yameshapatikana, hivyo yanasubiriwa majibu ya kipimo kingine ili aweze kuanza rasmi matibabu, lengo likiwa ni kubaini kitaalamu ugonjwa unaomsumbua.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KOCHA MARSH ASUBIRI VIPIMO VYA MWISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top