• HABARI MPYA

    Monday, February 03, 2014

    AZAM FC WAINGIA KAMBINI KUWAWEKEA AKILI SAWA WAMAKONDE

    Na Dina Ismail, Dar es Salaam
    BAADA ya kuibuka na ushindi mnono wa magoli 4-0 dhidi ya Kagera Sugar, kikosi cha Azam FC kesho asubuhi kitaingia kambini jijini Dar es Salaam kujiandaa kwa mechi ya kwanza ya Hatua ya Awali ya mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Ferroviario de Beira ya Msumbiji itakayopigwa Uwanjja wa Azam mwishoni mwa wiki.
    Kocha msaidizi wa Azam FC, Kalimangonga Ongala 'Kally' ameiambia BIN ZUBEIRY jijini Dar es Salaam leo kuwa baada ya mechi ya jana, wachezaji walipewa mapumziko ya siku moja na kesho wataanza rasmi mazoezi kwa ajili ya mechi hiyo.

    "Tumefurahi kwa sababu tumeshinda mechi dhidi ya Kagera Sugar na kuendelea kuongoza ligi ligi lakini kikosi chetu bado kina upungufu kidogo katika kumalizia nafasi tunazozitengeneza. Leo (juzi) Kagera hawakuwa vizuri, hatukupaswa kuwafunga magoli manne tu, tulikuwa na uwezo wa kuifunga magoli nane lakini wachezaji wakajisahau," amesema Kally na kuongeza: 
    "Unapotengeneza nafasi kisha unashinda kuzitumia vyema ni hatari kwa sababu pale unapocheza na timu ambayo iko vizuri, lazima iotakuumiza. Tutazifanyia kazi kasoro hizo kabla ya kuanza kwa mshindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika. Leo tunapumzika, kesho tutaanza mazoezi rasmi kwa ajili ya Kombe la Shirikisho."
    Azam, ambao msimu uliopita pia waliiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo baada ya kumaliza wa pili ligi kuu, wakifanikiwa kuitoa Ferroviario watamenyana na mshindi kati ya St. Michel ya Shelisheli na ASSM Elgeco Plus ya Madagacar.
    Wakati Wanalambalamba wakitangaza kuanza mazoezi rasmi kesho, uongozi wa Yanga kupitia kwa Ofisa Habari wake, Baraka Kizuguto umesema kuwa kikosi chake ambacho kinaiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Klabu Bingwa Afrika, kitaingia kambini mjini Bagamoyo kesho asubuhi kuanza kuandaa dozi kwa ajili ya mechi ya kwanza Hatua ya Awali ya mashindano hayo dhidi ya timu ya Komorozine de Domon kutoka Comoro itakayopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumamosi.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC WAINGIA KAMBINI KUWAWEKEA AKILI SAWA WAMAKONDE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top